UNYAMA wa
kutisha! Gasto Edward (32) amemkata mkewe Mwelu Raymond sehemu zake za
siri, Risasi Jumamosi lina simulizi hii ya kusikitisha. Tukio hilo
lilitanguliwa na kumpiga mkewe huyo na kipande cha nondo kichwani hali
iliyosababisha apoteze fahamu papo hapo na kutekeleza azma yake.
Imeelezwa kuwa, tukio hilo lenye sura ya
majonzi, lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Jumatano ya wiki hii,
huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
KISA CHA YOTE
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke aliyejulikana kwa jina la Mgogo.

Chanzo chetu cha kuaminika, kwa sharti
la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu na Gasto wametoka mbali, wameishi
kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto wawili, sema siku za hivi
karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa.
Wananchi wakiwa eneo lilipotokea tukio hilo.
“Tena siyo tuhuma, anasema alikuwa
akimwambia wazi kuwa ana mwanaume wake Mgogo ambaye yupo Temeke. Jamaa
alikuwa analalamika kuwa mkewe alifikia hatua ya kumwambia amuache ili
aende kwa mwanaume huyo anayejua kutunza.”
Akaongeza: “Unajua katika hali ya
kawaida, kama ni kweli mke alikuwa akimwambia mumewe maneno ya hovyo
kama hayo, yanaumiza. Ndiyo maana jamaa akaona kwa sababu chanzo cha
yote ni penzi, akamkata nyeti zake.”
MJUMBE ANAFAFANUA
Mjumbe wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
Mjumbe wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
Ujumbe alioandika bwana Gasto kabla ya kutokomea.
“Ni kweli walikuwa na tofauti na hili
suala lilinifikia hata mimi. Gasto alikuja kulalamika kuwa mkewe siyo
mtulivu na anamwonyesha dharau. Lakini tulisuluhisha yakaisha. Jana
(Jumatano) ambapo tukio lilitokea, yule mkewe alikuja kulalamika kuwa
mumewe amebadilika.
“Alisema amemuona akinoa kisu asubuhi,
usiku ugomvi ukatokea akaamua kuja kulala kwangu, lakini baadaye
akaniaga anakwenda kulala kwa jirani yao mama Mbonde, huko ndipo mumewe
alipokwenda kumchukua na kumfanyia unyama huo.”
WOSIA MZITO
Baada ya tukio hilo, Gasto alitoroka lakini aliandika wosia uliomtaja mrithi wa mali zake kuwa ni watoto wake Edward na Editha ambapo alimchagua kabisa msimamizi wao kuwa ni mdogo wake aitwaye Kiriani.

Jalada alilofunguliwa Gasto.
Katika barua hiyo, Gasto alisema
anakwenda kujiua kwa sababu amechoshwa na dharau za mkewe, ndiyo maana
akaamua kuondoa sehemu zinazompa kiburi.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa na Risasi Jumamosi ili kuelezea
tukio hilo, alikiri kupokea taarifa, akasema bado wanafuatilia.