NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya
viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze
sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo
huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia
mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.
Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo
yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye
tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa
mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.
Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato
cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa
wa 8 na 9 na pia unaweza kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya
sekondari au kwenye ofisi za elimu za mkoa na wilaya.