Ntaa wa sinema za Bongo asiyetabirika maisha, Aunt Ezekiel
Kwa mujibu wa chanzo, nyota huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki
iliyopita jijini Dar baada ya kutua toka Dubai alikodai alikwenda kwa
mume wake.Ilidaiwa kwamba, mara baada ya kutua Bongo, Aunt alikutana na shoga yake mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja na kutonywa kuwa kuna gazeti liliandika habari yake kwamba wakati mumewe akidaiwa kuwa jela, yeye anaponda raha Dubai.
“Aunt aliambiwa kuwa wasemaji wakubwa wa maneno hayo ni ndugu wa mumewe yaani mashemeji na mawifi zake. Wao wamesema watawasiliana na mume wake kule aliko, hata kama ni gerezani, atoe kibali cha ndugu yeyote wa kiume kuandika talaka na kukabidhiwa Aunt kwa vile hana uchungu na matatizo ya mumewe.
AUNT ASHTUKA KWA MANENO YA NDUGU WA MUME
“Taarifa hizo zilimshtua sana Aunt mpaka akaonekana kupaniki, akajibu mapigo kwa kusema ‘niko tayari kwa talaka, kwanza mimi mwenyewe ndiyo naomba wanipe talaka. Kama hao ndugu wanaweza kwenda kwa Demonte wakapewa kibali cha kunipa talaka basi mimi nasema naomba wanipe’ niko tayari,” kilisema chanzo hicho kikimkariri shoga wa Aunt.
Staa wa sinema Aunt Ezekiel akiwa na mumewe wakati wa ndoa yao
SHUTUMA NYINGINE KWA AUNTAma kweli ndoa ndoano, Aunt amekuwa akitupiwa shutuma kibao kutoka kwa baadhi ya ndugu wa mumewe (baadhi lakini) kwamba mke huyo wa ndugu yao hana ushirikiano na wanafamilia kama vile kuwatembelea, kuwajulia hali na hata kuwatupia chochote kitu pale anapokuwa amepata.
“Aunt tangu ameolewa mwaka juzi hajawahi kuja kwangu, mimi namwona kwenye filamu tu. Sijui ni kwa nini Demonte alimuona anafaa kuwa mke wake. Lakini kwa vile kupenda ni moyo, sina usemi,” alisema ndugu huyo ambaye aliomba asichorwe gazetini.
AUNT ASAKWA
Juzi, Amani lilimtafuta Aunt kwa njia ya simu yake ya mkononi ili ajibu madai hayo lakini hakupatikana hewani.Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia gazeti hili kwamba Aunt huwa hapatikani kwenye simu kuanzia saa kumi alfajiri hadi mchana unaofuatia kwa sababu akisharudi nyumbani na kulala huamka mchana jua likiwa utosini.
Mapaparazi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala na kuambiwa hakuwepo na msichana aliyekutwa kwenye makazi hayo.
Amani: Hayupo kasafiri au?
Msichana: Hayupo tu!
Amani: Kuwa muwazi basi.
Msichana: Kwani kusema Aunt hayupo ni usiri?
Baada ya waandishi wetu kuondoka, ilibainika kwamba Aunt ana tabia ya kulala nje, kama si kwa staa mwenzake Wema Sepetu (Mwananyamala, Dar) basi kwa shoga yake kipenzi, Nice Chande (Changanyikeni, Dar).
Amani lilimwendea hewani kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini iliita kwa muda bila kupokelewa. Ilikuwa saa 9:25 alasiri.
Baada ya dakika tano, Amani lilimpigia tena ambapo alipokea. Baada ya salamu, madai yakaanza.
Amani: Inasemekana umedai talaka kutoka kwa mume wako baada ya kusikia manenomaneno kutoka kwa mashemeji zako halafu swali jingine…
Aunt: Sitaki jamani sitaki. Ndoa yangu naomba ipumzishwe. Kwanza naomba kusema kwamba, mimi sijasema kama nimepewa talaka au sijapewa. Ni uamuzi wangu kusema.
“Kwa sasa sijasema lolote, siku nikitaka nitasema. Kwani mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kupewa talaka? Hebu nipumzisheni. Andikeni kuhusu filamu zangu.”
Amani: Filamu yako ipo?
Aunt: Siku ikitoka.
Amani: Basi siku ikitoka tuambie tutaandika.
Aunt: Siyo lazima niwaambie, nyie wenyewe mtaona imetoka