SIKU tatu
baada ya serikali kutangaza mfumo mpya wa madaraja ya ufaulu, licha ya
kupingwa na wengi, kitendo hicho pia kimemhuzunisha Katibu Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, Dk. Slaa alisema: “Kwa kubadili mfumo wa maksi
serikali sasa bila huruma imeamua kwa makusudi kabisa kuua ubora wa
elimu nchini, ni kweli kwa kupanua wigo wa kufaulu serikali haitalaumiwa
kwa akili ya kawaida, itaonekana wamefaulu wote, lakini elimu
haitawasaidia watoto wenyewe, haitawasaidia wazazi wenyewe, na
haitasaidia taifa letu. Tutapataje madaktari bora, tutapataje
wanasayansi, walimu au wahandisi bora? Mabadiliko yanahitajika kusaidia
taifa hili lisizikwe na watu wasio na huruma.”
Kwa upande
wake, Dk. George Kahangwa, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akizungumza kupitia kipindi cha ‘Tuongee’ kinachorushwa na Star TV,
alisema hatua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome,
kutangaza mageuzi hayo ni kuonesha ni jinsi gani serikali imeshindwa
kutatua mzizi wa tatizo la elimu nchini na baadala yake inatapatapa kwa
kuja na sera iliyoiacha kuitumia toka mwaka 1995 iliyotumia alama hiyo
ya 50 kwa 50 kwa Tanzania Bara na 40 kwa 60, kwa Visiwani Zanzibar
ambapo safari hii imeamua kuitumia tena na kuiweka wazi.
Dk.
Kahangwa alisema serikali licha ya kutoa tamko la kubadilisha daraja
jipya huku ikikiri kuwa ilikuwa ikitoa alama za kuanzia 75 hadi 100 ndio
ufaulu wa alama ‘A’ na daraja la kwanza, pasipo kuiweka wazi kwa muda
mrefu, sasa wameamua kuiweka wazi, huku ni kuwaada Watanzania kwa
kutumia sera ambayo hazitekelezeki.
“Hili ni
janga la elimu, huko nyuma waliondoa ‘sifuri’ kwenye ufaulu na kuweka
‘feli’, leo hii wanakuja tena na kuongezea daraja la tano na kuita
‘ufaulu hafifu au ufaulu usioridhisha’, huku ni kucheza na masuala ya
msingi katika taifa. Kuja mbele za umma na kutangaza tena juu ya sera
hiyo waliyoiacha kwa muda pasipokuitumia ni jinsi gani sera hiyo
haitekelezeki tena,” alisema Dk. Kahangwa.
Dk.
Kahangwa amewaomba Watanzania na wadau wa habari nchini kujitokeza
kuwahoji wadau wa elimu kama walishirikishwa kwenye kupitishwa kwa
mabadiliko hayo.
Dk.
Kahangwa alisema hivi karibuni kuna shirika lilifanya utafiti wa shule
za sekondari 100 ambapo shule nne tu ndizo zinahesabika kama shule bora
huku 96 zikihesabika kama makambi ya shule.
Hata
hivyo, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo,
aliyekuwapo kwenye mahojiano hayo alifananisha kitendo cha serikali
kupanga madaraja hayo kuwa ni sawa na kupanua magoli ya uwanja ili kila
mchezaji afunge, huku akiitaka serikali iwaombe radhi wananchi kwa kuwa
ilianza kutumia mfumo huo bila kuwaarifu.
Naye
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, Edwin Soko,
alisema mabadiliko haya yaliyolenga kuongeza idadi ya wahitimu bila
kuangalia uzoefu, yamesababisha taifa kukosa falsafa na Dira ya Taifa