Pichani juu ni malkia wa mipasho Khadija Kopa akiwa stejini katika usiku wake maalumu, huku akisindikizwa na kundi zima la TOT.
Kiongozi wa TOT, Gasper Tumaini, akiushukuru uongozi wa Dar Live kwa kuandaa usiku wa Malkia muda mfupi kabla hajapanda stejini
Mkurugenzi
wa Dar Live Masha James (kushoto) akimkabidhi Kopa bahasha yenye kitita
cha shs milioni moja usiku wa kuamkia leo ndani ya Usiku wa Kumtoa
Malkia, Dar Live.
MALKIA
wa Mipasho Khadija Kopa, usiku wa leo ameibuka kwa mara ya kwanza na
wimbo mpya uitwao 'A Lady with Confidence' katika kiwanja cha burudani
cha Dar Live, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuimba baada ya kukaa ndani
eda kwa muda wa miezi minne na siku 10. Wimbo huo, ambao unaonekana kuwa
moto wa kuotea mbali, ameuimba katika onesho lake maalumu la kumtoa nje
na umemuwezesha pia kupewa kitita cha shilingi milioni moja na uongozi
wa Dar Live, pesa iliyokabidhiwa kwake na Mkurugenzi wa Dar Live na
Global Publishers, Masha James.
PICHA: RICHARD BUKOS/GPL