Huku matokeo ya mwisho ya
uchaguzi mkuu yakisubiriwa, tume ya uchaguzi ya Zimbabwe inasema chama
cha Rais Robert Mugabe, ZANU-PF, kimepata thuluthi mbili za viti.
Mpinzani mkuu wa ZANU-PF, chama cha MDC, kimekuwa na kikao kuamua mikakati ya siku za usoni.
MDC inasema haitakubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu ya udanganyifu mkubwa katika upigaji kura.
Inaarifiwa kuwa afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amejiuzulu, na ametaja ulalamishi katika kura.
Makundi mawili ya Afrika ya wasimamizi wa uchaguzi, kwa jumla yameunga mkono uchaguzi ingawa yameeleza wasi-wasi kuhusu idadi ya wapigaji kura bandia, na kwamba baadhi ya wapigaji kura hawakuruhusiwa kupiga kura.