PENNY "MIMI NA DIAMOND HUWA TUNAMSIKILIZA YOUNG KILLER"

young killa picNani alijua kuwa miongoni mwa nyimbo anazopenda kusikiliza ‘The Bongo Flava Prince’ Diamond Platnumz ni za Young Killa?
Kwa mujibu wa mchumba wake Diamond, Penniel Mungilwa aka Vj Penny, wote kwa pamoja ni mashabiki wakubwa wa rapper huyo mwenye umri mdogo lakini aliyejaaliwa uwezo mkubwa wa kuandika mashairi ya hip hop.....
Penny ameimbia Bongo5 kuwa mara nyingi wamekuwa wakisikiliza single ya kwanza ya rapper huyo kutoka Mwanza, Dear Gambe.

ae580d60e65c11e2bf4822000a1ddbe2_7 Penny

Bongo5 ilitaka kufahamu reaction yake kuhusu wimbo mpya wa Young Killa, Mrs Superstar iliyoachiwa jana ambayo Penny ni miongoni mwa wasichana waliotajwa.

“Sasa vipi ningekuwa na Penny, hivi ntakuwa free au kama ningekuwa na Mwasiti wa THT, Ila Penny nahisi Diamond atanisumbua hata Mwasiti najua Pendo langu atalivua,” anarap Killa.

Kwa mujibu wa Penny, Young Killa ndiye msanii bora kabisa wa Hip Hop kutokea katika kipindi cha miaka michache iliyopita nchini Tanzania.

back to top