HAUSIGELI ABAKWA, ALAWITIWA

 
KWELI dunia haina huruma! Msaidizi wa kazi za ndani ‘hausigeli’ mmoja (jina tunalo), mkazi wa Chanika, Dar, anadaiwa kubakwa na kulawitiwa na mwanaume kwa muda wa miezi minne mfululizo, Risasi Jumamosi limeichimba.
Habari zilidai kuwa binti huyo mwenye umri wa miaka 15, mwenyeji wa Masasi, Mtwara alifika jijini Dar mwaka jana kama hausigeli maeneo ya Mbagala, Dar.
Ilifahamika kuwa Machi, mwaka huu ndipo alipokutana na mwanaume huyo aliyemdanganya kuwa amemtafutia kazi yenye mshahara mnono maeneo ya Chanika na kumuachisha kazi alipokuwa akifanyia mwanzoni.
Ilidaiwa kuwa alipofika Chanika, alishangaa kuona amepangishiwa chumba na kuanza kufanyiwa ukatili huo hasa kuingiliwa kinyume na maumbile huku akikatazwa kusema chochote kwa majirani, jambo ambalo alilitekeleza kwa hofu hadi pale alipozidiwa na maumivu kiasi cha kushindwa kutembea.
Uchunguzi wetu ulibaini kuwa mwanaume anayetuhumiwa kufanya jambo hilo baya katika jamii anatajwa kwa jina la Godlove Gasper (44) ikidaiwa ni mlinzi wa Kampuni ya Tool Security ya jijini Dar.
Habari zilisema kuwa jamaa huyo ana mke na watoto watatu huku mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 15, sawa na huyo hausigeli.
Wakizungumza kwa hasira, majirani walisema kuwa binti huyo alikuwa akifungiwa ndani muda wote huku mwanaume huyo akionekana nyakati za mchana akiingia ndani ya chumba hicho na kutoka baada ya muda akiwa na vitambaa vya binti huyo vyenye vinyesi ambavyo alikuwa akivifua na kuvianika, jambo lililowashtua wengi kuwa kumbe alikuwa akijisaidia humohumo.
Akisimulia yaliyomkuta, binti huyo alisema kuwa mwanaume huyo alikuwa akivitumia vitambaa hivyo kumkanda michubuko na vidonda sehemu zake za siri kila mara kabla ya kumuingilia hadi majirani waliposhtuka na kutoa msaada.
Baada ya ushirikiano mzuri wa majirani na polisi, mtuhumiwa huyo alinaswa Julai 21, mwaka huu na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Sitakishari-Ukonga, Dar na kufunguliwa faili la kesi namba STS/RB/13571/13- KUBAKA.
Wakati jamaa huyo akisubiri kupandishwa kizimbani, binti huyo alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilala ya Amana ambapo bado anaendelea na matibabu.
back to top