Akiwa na miaka 89 Robert Mugabe ambaye aliingoza nchi ya Zimbabwe
kupitia kwenye mdororo wa uchumi mkubwa zaidi kutokea kwenye nchi hiyo,
ameshinda tena kwa mara ya
saba kiti cha
urais. Unaambiwa licha ya tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza kwamba
Mugabe ameshinda kwa asilimia 61, mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai
amekataa matokeo ya uchaguzi huo.
Upande wa viti vya ubunge, chama cha
ZANU PF kinachoongozwa na Mugabe kimeshinda theruthi mbili ya majimbo
yote kitu ambacho kinamuongezea ngumu mugabe huko bungeni.
Nchi za magharibi zimesema kwamba wana wasi wasi kama uchaguzi huo ukukuwa wa ukweli na haki.