Kutokana na foleni kubwa ambayo imekuwa tatizo kwa wakazi wa Dar es
salaam hasa wenye shughuli zinazowalazimu kufika mjini, serikali
ilianzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi ikiwa ni moja ya mipango ya
kuepesha foleni na kuwafikisha watu kwenye maeneo yao ya kazi ndani ya
muda.Mradi huo umeanza na ujenzi ambao unaweza kuonekana hasa kwenye
barabara ya Morogoro, hii hapa ni update jinsi mradi huo unavyoendelea
hivi sasa kuanzia stendi kuu pale Jangwani hadi Kimara mwisho. Cheki
picha na
maelezo yote
Ukifika Jangwani hii ndiyo view ya mjini kama unavyoona kwa mbali
Bango la ujenzi unakutana nalo ukiwa unaingia kwenye site ya kituo kikubwa
Muonekano wa mbele wa jengo la kituo kikubwa cha mabasi yaendayo kasi
Closer view
Unaambiwa hapa ndiyo ndani ya jengo na kutakuwa na migahawa na bar kwa ajili ya abiria kusubilia mabasi yafike
Ukiwa bar au restaurant, hii ndiyo view yako ambayo ni parking ya mabasi yenyewe. Basi likifika unaenda zako kupanda
Mabasi yatakuwa yanajipanga hapa
Pembeni ya jengo kuna ofisi na garage ya hayo mabasi
Ujenzi bado unaendelea na mashine zipo zinafanya kazi
Haya mabomba yanatumika kujenga mfumo mzuri wa maji taka kwasababu mitalo mingi imefukiwa ili barabara ijengwe.
Ilikuwa ni jumapili lakini kazi inaendelea kama kawaida
Ukitoka Jangwani ukafika mbele kidogo Magomeni Usalama, kituo kishawekwa hadi kibao cha utamburisho wa kituo.
Mtu wangu wa nguvu, hapohapo Magomeni pia kuna tawi la NMB Bank. Unaweza kufika na kujipatia huduma za kibenki pia.
Vituo vya haya mabasi ni virefu kama unavyoona mwenyewe
Safari
ilifika Manzese, huu ni muonekano wa maendeleo ya barabara kutoka
kwenye daraja la Manzese. Unaweza kuona kituo kwa mbali.
Upande wa pili wa daraja la Manzese na barabara inaonekana kuendelea vizuri
Haya magari yanafanya kazi za mfumo wa maji taka pembeni ya daraja la Manzese
Ukiwa kwenye lile daraja unaweza pia kuliona jengo la Milleniums tower kwa mbali sana kama unavyoliona
Safari
ikafika Ubungo, kuna vitu vinafanyika kwenye huu ujenzi kwa mtu ambaye
siyo mtaalamu au haujaiona ramani ya ujenzi huu. Huwezi kuelewa kirahisi
ni nini wanafanya,mfano hapa sikupata hata mwenyeji wa kunielezea ni
kitu gani hiki.
Ubungo stand ya mkoa hapo.
Bado tupo Ubungo
Hili
ni kitu kama daraja linajengwa, mara ya mwisho napita hapa halikuwepo.
Leo nimeona mabadiriko kitu ambacho kinaonyesha ujenzi unaenda vizuri.
Upande huu unaungana na stendi ya mkoa.
Ukitoka Ubungo, ujenzi mwingine utaukuta Kimara ambapo kuna kituo kikubwa sana kinajengwa