Magna
Carta Holy Grail album ya Jay Z bado ipo kwenye headlines, kitu kikubwa
sasa hivi ni video ya performance ya “Picasso Baby “. Jay Z alitoa
video ya dakika 10 ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Perfomance Art
Film na imekuwa gumzo kwenye internet.
Kitu ambacho watu wengi hawajakitambua ni kuhusu uhusika wa raia wa Kenya kwenye video ya Picasso baby. Msanii Wangechi
Mutu amezaliwa mwaka 1972 na kazi zake nyingi anazifanya Brooklyn New
York. Wangechi ni moja kati ya wachoraji wenye heshima kubwa kutoka
Africa wanaofanya kazi nje ya Africa. Mutu licha ya kuwa msanii ni msomi
wa Masters ya Fine Arts kutoka Yale University. Soma zaid kuhusu Mutu HAPA