Elias Peter wakati akiongea na wanahabari wetu (hawapo ichani). Msikilize katika video hapa chini:
Akizungumza na paparazi wetu, Elias alisema siku ya tukio alipewa sigara na kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Saleh Mtima alipomaliza kuvuta alianza kuhisi baridi kali ghafla akajishtukia uume haupo amebaki ‘flat’.
Baada ya hapo alikaa siku tatu bila uume kurudi ndipo akaamua kwenda kumueleza na kumuomba ushauri mzee mmoja anayeheshimika sana eneo hilo anayejulikana kwa jina la Mfinanga Kishegwe akamweleza kuwa kilichompata ni mashetani ila uume utarudi.
“Baada ya kusubiri kwa siku tatu nilienda kuomba ushauri kwa mzee Mfinanga ambaye aliniambia utarudi na baada ya muda kweli ulirudi lakini ulikuwa mdogo kama wa mtoto na haukuwa na nguvu jambo ambalo limepelekea pale mtaani ninapoishi kila nikipita watu wananizomea na kuniita mwanamke,”alisema Elias.
(Habari/Picha/Video : Na Gladness Mallya / GPL)