“Nafurahi kuona jinsi kioo cha jamii hivi sasa kimeigusa familia kabisa, ukizungumzia nyumba unagusa swala la familia ambalo ndiyo msingi wa Taifa lolote.” Haya yalikuwa ni baadhi ya maneno ya Mtitu, mmoja kati ya watu maarufu ambao walihusika kwenye show ya Irene Uwoya.
Katika harakati za kutengeneza kipindi chake, Irene amekutana na mastaa tofauti na kuzungumza nao mambo mengi ambayo yatakuwa kwenye show yake. Chukua time yako ya kuona jinsi ilivyokuwa na upate sababu nyingine ya kuangalia hii show kupitia @CloudsTV na pia unaweza kucheki promo yake hapo pembeni.