Hivi
karibuni mitandao ya nchini Kenya iliandika tetesi kuwa huenda Miss
Kenya wa sasa, Shamim Nabil anadate na Mr. Nice aliyehamia nchini humo
na kwamba walionekana na paparazzi wakila bata pamoja.
Kutokana na tetesi hizo, Shamim ameamua kuzungumza na kukanusha kuwa kamwe hawezi kuwa mpenzi wa Nice Mkenda.
Amesema amekuwa akimfahamu staa huyo tangu akiwa mdogo na Nice si mwanaume wa aina yake.