Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti nijambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yakeutajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume kwa sababu tu yakuendekeza hisia mbaya. Acha kuhisi, tafuta ukweli.
2. TUTAACHANA
Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”. Wanafanya hivyoeti kwa kutafsiri mwenendo usioridhisha wa mapenzi yao. Kusema kweli hili nijambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala yakwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana namwenzako kila siku.
3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi. Hata kamahawajaambiwa chochote kuhusu kutowatosheleza wenza wao faragha,hukimbilia kujihukumu.
Hujaambiwa kama umecheza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kamauna lolote linalokufanya uwe na hofu muulize mwenzio.
4. NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maanahawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji. “Yaani mimi ningekuwa kamafulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.”
Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya. Jisahihishena epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
5. NITAMUUA
Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwasababu yoyote. “Nikimfumania na mwanaume mwingine nitamuua.”
Mtu anayetawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka katika mtego mbayakisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anachojiapiza hata kwa sababu ndogo.Usifikirie hivyo maishani mwako.
6. NIMEKOSEA KUCHAGUA
Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwakasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kulikokuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko hivinisingemchagua.” Usiwaze hivi!
7. HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtotohufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa nne umepita bilamtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.”
Kwa nini msizae? Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwazehivyo? Jipe moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wamwaka mmoja?
8. UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusemana kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo licha yakuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hilini jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi unadanganywa, utapotezabahati yako.