Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania ametembelea makao makuu ya shirikisho la
soka duniani FIFA hapo jana ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na
Rais wa shirikisho hilo Joseph Sepp Blatter.
Amenukuliwa akisema.
“Namshukuru Rais President Blatter kwa mwaliko wake wa heshima hapa
makao makuu ya FIFA nyumbani kwa mchezo ambao wote tunaupenda"
"Nampongeza
pia Rais Blatter kwa kazi kubwa ya kuendeleza soka tangu aingie katika
kazi yake, mchezo huu umeleta maendeleo makubwa na kupiga hatua kubwa."

"Pia
nakubalina na nia yake Rais Blatter aliyoionyesha ya kuendeleza soka
barani Afrika ni kutokana na juhudi zake ndio maana leo Afrika inaingiza
timu tano katika fainali za kombe la dunia kama ilivyokuwa fainali
zilizo pita 2010 katika ardhi ya Afrika.
Rais Kikwete
amesema Tanzania imekuwa ikipokea misaada mingi kutoka FIFA kwa miaka
mingi, na anatarajia hilo litaendelezwa mpaka vijana wa Kitanzania wote
wakiume na wa kike watakapo kuwa wameingia katika mchezo huo.
Amesema
kwa bahati mbaya kwasasa Tanzania inapigana kuhakikisha inafika katika
kiwango cha juu cha soka la dunia lakini uvumilivu unahitajika na
mafanikio yatakuja na anaamini katika hilo.
Rais
Kikwete ambaye ni mchezaji wa zamani wa mchezo wa Kikwete pia ni mpenzi
mkubwa wa soka mchezo ambao unapendwa na watu wengu duniani.
Amekaririwa akisema
“Nimecheza
mpira wa kikapu na soka , lakini nilipenda sana kikapu mchezo ambao kwa
kiasi fulani nilionyesha kipaji changu, ndio maana niliambiwa nijitume
zaidi katika mchezo huo kuliko soka ambao niliwaacha wenzangu wazuri
katika mchezo huo waendelee, nadhani nilifanya uchaguzi sahihi”
Tukirudi
nyuma katika suala la ulinzi wa amani barani Afrika hususani katika
ukanda wa maziwa makuu hususani Burundi na Congo DR, Rais Kikwete akiwa
huku amesema anaamini soka ina nguvu kubwa ya kuleta amani na kuwaleta
watu pamoja.
Amenukuliwa akisema
"Soka inaeweza kutoa mchango mkubwa katika suala la amani"
Amesema
"Hata
kama nchi iko katika vita watu wanacheza soka hata kwa mataifa ambayo
yako katika hali ya kiurafiki kisiasa au kidiplomasia, mara nyingi
wanajikuta wakicheza katika dimba la soka, na hakuna matatizo."Hiyo ni
kauli ya Rais Kikwete huko FIFA.