Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu,Flossy Gomile-Chidyaonga.
Jeneza lenye mwili wa Balozi Flossy Gomile-Chidyaonga likiwa mbele ya waombolezaji.
Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossy Gomile-Chidyaonga enzi za uhai wake.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha waombolezaji.
Mkuu
wa Chuo cha Kijeshi na Maofisa Waandamizi wa Serikali kilichopo
Kunduchi, Dar, Luteni Jenerali Makakala akisaini kitabu cha maombolezo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akiwasili katika
Viwanja vya Ukumbi wa Mwalimu J.K Nyerere kuaga mwili wa Balozi Flossy
Gomile-Chidyaonga.
Wanakwaya kutoka Malawi wakiimba wakati wa ibada.
Maofisa wakishiriki ibada ya kumuombea Balozi Flossy.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali.
Maofisa kutoka Malawi wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa kuaga mwili wa marehemu.
Waziri Membe akitoa pole kwa maofisa kutoka Malawi.
Mwili wa marehemu wakati ukiagwa.
Dkt. Bilal akiagana na maofisa kutoka Malawi baada ya zoezi la kuaga.
MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal ameongoza waombolezaji kuaga mwili
wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossy Gomile-Chidyaonga
katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.Viongozi mbalimbali wa nje na ndani ya nchi wamehudhuria zoezi hilo la kuaga mwili wa balozi Flossy aliyefariki dunia Ijumaa, Mei 9 mwaka huu baada ya mshipa mkubwa wa Aorta kuvimba na kupasuka.
Mwili wa marehemu Chidyaonga unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumanne kwenda Malawi na Jumatano mazishi yamepangwa kufanyika huko Blantyre, Malawi.