JOKATE AHOFIA HOMA YA DENGU

MWANAMITINDO maarufu Bongo ambaye pia ni Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Channel O cha Sauzi, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameweka wazi hofu aliyonayo juu ya gonjwa hatari la Homa ya Dengu ambalo limeshika kasi katika jiji la Dar es Salaam.

 
Mwanamitindo maarufu Bongo ambaye pia ni Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Channel O Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
Akizungumza na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema anapata wakati mgumu sana  anapohisi anaumwa kwani huamini kuwa tayari amenasa homa hiyo.
“Ninauogopa sana huu ugonjwa wa Dengu maana nasikia ni hatari sana, basi mimi nikiumwa kidogo tu nahisi ndio tayari nimeukwaa na sijui hata unatibiwa vipi, naogopa sana kufa,” alisema Jokate.
back to top