Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper ambaye ana muonekano wa
‘kigumu’, alisema siku zote anaamini katika kupambana hivyo hawezi
kumlilia mwanaume hata iweje.“Sijawahi kulia pale nilipoachwa wala kuachana na mwanaume, akili yangu yote inaamini katika kutafuta maisha hivyo siwezi kujirahisisha nikamwaga machozi kwa ishu za mapenzi,” alisema Wolper.