JB ATESWA NA MAJUNGU

BABA la baba, Jacob Steven ‘JB’ amenyanyua kinywa chake na kutamka kuwa anateswa na majungu katika fani hivyo angekuwa na mbadala wa kazi, angechepuka.

 
BABA la baba, Jacob Steven ‘JB’
Akistorisha na gazeti hili hivi karibuni, JB alisema licha ya umri wake mkubwa katika tasnia ya filamu lakini suala la majungu limekuwa likimtesa na mbaya zaidi ni ngumu kulidhibiti.
“Kusema ukweli majungu ni mengi kiasi ambacho kungekuwa na mbadala wa kazi ningefanya ili niwaache na majungu yao ya kila kukicha,” alisema JB.
back to top