Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Batuli alisema licha ya
kuwa walimwagana na staa huyo lakini hatokuja kupenda mwanaume kama
alivyompenda Mtunis.“Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni mara moja tu mengine tutadanganyana,” alisema Batuli.
Hivi karibuni Batuli aliripotiwa kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha ajabu mtoto wa kike hakuonesha dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.