“Lakini nashukuru Mungu sana kuona nimependeza na kila mtu anataka kupiga picha na mimi pamoja na fundi kunifanyia mtima nyongo, amenitibua kweli,” alisema Davina aliyetinga ukumbini na gauni nyeusi.
Mwigizaji wa Filamu bongo, Vanitha Omari akilia kwenye kitchen party yake.
MALISA AIBUA KILIO UPYA UKUMBINIWAGENI mbalimbali waalikwa wamejikuta wakiangua vilio upya baada ya kumkumbuka aliyekuwa mwigizaji, Zuhura Maftah ‘Melisa’.
Tukio lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mawela, Sinza jijini Dar wakati dada wa marehemu (Haris) alipokwenda kutoa zawadi kwa niaba ya marehemu kwenye kitchen party ya mwigizaji Vanitha Omari.
“Mungu alimpenda zaidi mdogo wangu kabla hajafanikisha zoezi hili ila nimeamua nimtolee zawadi rafiki yake kwani alipanga kumchangia Vanitha,” alisema Haris na kusababisha biharusi mtarajiwa aangue kilio pamoja na baadhi ya waalikwa.
Melisa alifariki dunia mwaka jana baada ya kuugua na kulazwa kwa muda mfupi.