ARSENAL BINGWA FA, NI BAADA YA MIAKA 9 BILA KOMBE!

 
Arsenal wametwaa kombe la FA baada ya kukaa miaka tisa bila kombe lolote. Wametwaa ndoo hiyo kwa kuifunga Hull City bao 3-2 katika muda wa nyongeza baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida kwenye Uwanja wa Wembley usiku huu.

Wafungaji Arsenal: Carzola dakika ya 17, Koscielny dakika ya 71 na Ramsey dakika ya 109 wakati ya Hull City yakifungwa na Chester dakika ya 4 na Davies dakika ya 8.
back to top