Unaambiwa hili ndio litakuwa jengo refu zaidi duniani ikifika mwaka 2014

skycity980
Majengo marefu duniani yamekua kama alama na vivutio vya majiji mbalimbali ambapo mfano mzuri ni Hotel maarufu ya Burj al arab iliyojengwa ndani kidogo ya bahari kwenye jiji la Dubai.

Hivi sasa jengo refu duniani ni Burj Khalifa ambalo lipo Dubai na lina urefu wa mita 828 na unaambiwa ukifika mwaka 2014 ndio utakuwa mwisho wa utawala wake kwa kuwa jengo refu zaidi duniani kwa sababu sasa hivi huko China kuna jengo linaitwa Sky City One ambalo litakuwana urefu wa mita kumi zaidi ya Burj Khalifa na limeshaanza kujengwa.

130802032124-worlds-tallest-buildings-sky-city-horizontal-gallery
Majengo marefu duniani na urefu wake
Jengo hilo ambalo litagharimu zaidi ya ¥5.2 billion za kichina linakadiriwa kukamilika April 2014 na kuanzisha historia mpya ya jengo refu kuliko yote duniani.sky-city-one-04
Huu ni mchoro wa computer
back to top