KESI YA LADY JAYDEE YAKWAMA TENA

 
 Wakili wa Lady Jaydee, Mabere Marando (kulia) akimueleza jambo wakili wa viongozi wa Clouds Media Group, Ruge na Kusaga, Willy Lusajo. Katikati ni mume wa Anaconda, Gadna G. Habash.

 
Gadna akiondoka eneo la mahakama hiyo baada ya kesi kuahirishwa.
 
Gadna na Anaconda wakiwa ndani ya gari lao muda mfupi kabla ya kuondoka mahakamani.
KESI inayomkabili mwanamuziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ a.k.a Anaconda ya kuwakashifu baadhi ya viongozi wa kampuni ya Clouds Media Group, leo imekwama tena kusikilizwa baada ya hakimu aliyeshikilia kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Athuman Nyamlani kupatwa na hudhuru. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 6 mwaka huu mahakamani hapo.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyojiri eneo la mahakama hiyo.


( GPL)
back to top