VIJIMAMBO USWAZI

Afumwa akifuturu kwa nyumba ndogo!
Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukielekea ukingoni, njemba moja iliyotambuliwa kwa jina la Haji mkazi wa Charambe Magengeni Dar, hivi karibuni ilifumwa na mkewe ikifuturu kwa nyumba ndogo.
Habari kutoka kwa shuhuda wa kisa hicho zinapasha kwamba, tukio hilo lilitokea Julai 27, siku ya Jumamosi.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa, Haji ambaye ameoa na kujaliwa kupata watoto wawili ana nyumba ndogo aliyoipangia chumba Maji Matitu.
Aliongeza kuwa, tangu mfungo ulipoanza alikuwa akifuturu siku kadhaa nyumbani kwake na siku nyingine kwa nyumba ndogo yake.
“Kitendo hicho kilikuwa kikimkera sana mkewe ndipo Jumamosi aliamua kufuatilia nyendo zake, si akamfuma akifuturu kwa msichana huyo wa Maji Matitu, pakachimbika sana,” alisema shuhuda huyo.
Amkimbia mkewe kisa, penzi la kikongwe!
Jamaa aliyetambuliwa kwa jina moja la Kitwana mkazi wa Makole, Dodoma kamkimbia mkewe baada ya kunogewa na penzi la kikongwe aitwaye Koku.
Kwa mujibu wa mpashaji wetu, Koku anaishi maeneo ya Maili Moja mjini humo na kwamba uhusiano wao ulianza tangu mwaka jana.
Akisimulia zaidi tukio hilo kwa njia ya simu, mpashaji wetu alisema Kitwana aliamua kujiwekeza kwa kikogwe huyo ambaye ana wajukuu wa kutosha baada ya kuchoshwa na gubu la mkewe.
Mpashaji huyo aliongeza kuwa, mkewe hajui mapenzi ni nini, hamthamini na kumheshimu mumewe ndipo jamaa akaamua kujiweka kwa kikongwe huyo.
“Kero za mkewe zilipozidi jamaa kaamua kuhamia kwa kikongwe huyo ambaye anamlea kama mjukuu wake jambo lililomfanya anawiri,” alisema mnyetishaji wetu.
back to top