Ni siku kadhaa tu zimepita toka millardayo.com itoe ripoti kutoka Forbes ikiwahusu Watanzania Mohamed Dewji ambae ni Mbunge wa Singida mjini pamoja na mfanyabiashara Patrick Ngowi ambao walitajwa na hilo jarida.
Time hii ni Mtanzania Flaviana Matata, mwanamitindo ambae amekua akifanya kazi zake Marekani na Uingereza ambapo pamoja na kumiliki headlines kwenye Jarida kama hilo amewahi pia kumiliki headlines kwenye mitandao kadhaa mikubwa duniani ukiwemo wa Marekani wa Global Grind.
Basi pamoja na hayo ni kwamba Jarida hili limetoa list ya mamodo wa Afrika 2013 wenye ujazo katika wanachokifanya… ni furaha kuona Afrika Mashariki kwenye hii list mpya ya Forbes imewakilishwa na mwanamitindo pekee ambae anatokea Tanzania (Flaviana Matata) huku wengine waliobaki wanatoka Sudan, South Africa na Ethiopia.
Kwa nguvu ya Forbes, jina la Mtanzania limepenyeza mpaka kwenye blog maarufu ya Nigeria, taifa lenye nguvu kwenye burudani na uigizaji Afrika ambalo sio rahisi kwa Muafrika mwingine kupata nafasi ya kuonekana kwenye vyombo vyao vya habari lakini ripoti inayomuhusisha Flavvy imetokea bellanaija.com
Ukiguswa na hii post unaweza kutoa support kwa kutweet au kuiweka kwenye facebook mtu wangu wa nguvu na pia unaweza kumfollow @FlavianaMatata kwenye twitter na instagram ili kuwa karibu zaidi na info zake.