Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifanya vizuri sana kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini Congo DRC kwenye michuano ya kimataifa na amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi iliyochezwa jana kati ya timu yake ya Tp Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe ilishinda 3-0 na mpaka sasa Samatta amekuwa akifunga kwenye mechi zote nne za michuano hiyo ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya awe na nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.
Mbwana
Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao
walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na shauku ya kufahamu matokeo ya timu ya Tp Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu hiyo imeshinda au la na baada ya kuuliza hivyo huuliza tena Samatta amefunga mangapi kwa kuwa wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya kuzifumania nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa akiwa nchini Kongo ambapo mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye picha kila wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutaka kusukuma gari lake wanapoliona.