Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale jana aliwaaga
rasmi wachezaji wenzake ikiwa ni ishara ya kukaribia kwake kuihama klabu
hiyo kujiunga na Real Madrid ambapo kwenye kuaga huko aliweka saini za
kumbukumbu kwenye jezi zao walipokuwa wanapanda ndege kuelekea Ufaransa
ambako watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Monaco.
Bale alibaki nyuma jijini London ambako anamalizia sehemu za mwisho
za mazungumzo ya uhamisho wake kwenda klabu ya Real Madrid ambayo
imekuwa ikifanya juhudi za kumsajili na anatarajiwa kukamilisha usajili
huo ndani ya siku chache zijazo na inaaminika kuwa Madrid watalipa ada
ya uhamisho ambayo itavunja rekodi ya usajili.