Wakuu wa Sudan wanasema Rais Omar al-Bashir amezuwiliwa kuingia katika anga ya Saudi Arabia, na amelazimika kurudi Khartoum.
Saudi Arabia - ambayo ina uhusiano mbaya na Iran - haikutoa sababu ya kuchukua hatua hiyo.
Bwana al-Bashir anasakwa na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa vitani.
Mwezi uliopita al-Bashir alipewa heshima ya gwaride nchini Nigeria alipohudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika.
chanzo;bbc