MNAMO TAREHE 04.08.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO
MSWISWI WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA
SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA
HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA
MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA MKAZI WA MUNZE
LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO.
MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI
WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
|