Bomu hilo lilirushwa na watu
wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa
linazinduliwa na a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika
Akidhibitisha kutokea kwa tukio
hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa
tukio hilo lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe
wa kanisa hilo jipya
Sabas alisema kuwa wakati balozi
huyo anakata utepe huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo
liliweza kuwajerui watu huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja
“huyu balozi alikuwa hapa Arusha
toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa kutosha juu
yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu hali ambayo
ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo jipya”alisema Sabasi
Pia aliongeza kuwa mpaka sasa
polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini
uchunguzi unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini
pia msaada wa majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo.
wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa
Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa
wananchi wa jiji la Arusha hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio
hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano.
Alisema kuwa Serikali imejipanga
kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata matibabu ingawaje bado kuna
ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru)
“kazi ya uchunguzi tunatakiwa
kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa
Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali
kwani hawa majerui wameumia vibaya sana”alifafanua Magesa.
Wakati huohuo Mbunge wa jimbo la
Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya uharibifu wa
makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na Dar es Saalam
lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa sana ya watu
wafe.
Lema alisema kuwa lazima mambo
kama hayo yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu
kwenye makanisa hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna
hatari kama hiyo.
Aliyataka makanisa kuachana na
tabia ya kuwa karibu na wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa
wanajitegemea kwa michango yao wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi
kabisa kwenye makanisa.
Hataivyo Waumini waliojeruhiwa
katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za mount Meru, na
hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa
ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose
pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik,
Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji,
Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .
Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim.
Wakati huo huo jeshi la polisi
limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika
eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo
lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.