SABABU ZA KIUCHUNGUZI -'KWANINI WANAUME WENGI WANA MATATIZO KWENYE TENDO LA NDOA'

ASILIMIA 60 ya wanaume wasioweza kufanya tendo la ndoa inatokana na matatizo ya kisaikolojia. Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja wa Mradi wa Chama Cha Elimu ya Afya ya Uzazi cha Sweden (RFSU), Dk. Cathbert Maendaenda wakati wa semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyokuwa na lengo la kuzungumzia sheria ya masuala ya uzazi na ushiriki wa wananume. Dk. Maendaenda alisema wanaume wanaopata tatizo hilo kutokana na magonjwa, umri na maumbilie ni asilimia 40 tu.

“Kundi kubwa la wananume wanaopata tatizo hili si kwamba ni wagonjwa bali wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, ukiwaweka chini na kuwapatia elimu wanarudi katika hali yao ya kawaida.

“Lakini changamoto kubwa inayopata wanaume hawa ni kwamba hospitali zetu ninyi zimejengwa kwa mfumo wa kutoa tiba na si ushauri nasaha kwahiyo mwanaume anaweza kwenda kule ili kuelezea tatizo lake lakini kutokana na mazingira ya hizo OPD  anashindwa kujielezea.

“Matokeo yake anarudi nyumbani na kukaa na tatizo, kundi kubwa la wananume wa aina hiii wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji au kujitibu wenyewe kwa mitishamba wakiamini watapona lakini mwisho wa siku hakuna unafuu unaopatikana,” alisema Dk. Maendaenda.


Akizungumzia tatizo la usihiriki wa wanaume katika suala la uzazi alisema bado jamii ina changamoto kubwa kwasababu wanaume wanapewa haki za kufanya ngono zaidi kuliko wanawake.


“Kwenye jamii tunayoishi bado kuna tatizo kubwa, wanaume wamepewa uhuru wa kufanya ngono kuliko wanawake, mwanamke akimfumania mke wake jamii na familia inachukulia jambo hilo ni la kawaida.


“Lakini mwanaume anapokwenda kushitakiwa kwao au ukweni akisema nimemfumania mke wangu na mwanaume mwingine mwanamke huyo ataonekana nuksi na jamii itamtenge
“Sasa wote huu ni ukatili na kuminya haki za wanawake, ndiyo maana unaona mwanamke hata akijua mume wake anatoka nje ya ndoa ataishia kulalamika mwenyewe lakini hajui hatua za kuchukua,”alisema Dk. Maendaenda.

Alisema kutokana na hali hiyo ya kukandamizwa kwa haki zao, wanawake wengi waliko ndani ya ndoa wanashindwa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kutokana na kuwaogopa waume zao.
back to top