Mdomo wa Balotelli wamponza, apigwa chini na mpenzi wake.

MARIO Balotelli amepigwa chini na girlfriend wake Fanny Neguesha — siku kadhaa baada ya kusema kuwa kuwa timu nzima ya Real Madrid inaweza kulala naye kama ikisonga mbele kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya. Model Fanny, 22, aliamua kuondoka kwenye mjengo wa staa huyo nchini Italia kufutia ugomvi uliozuka baada ya Balo kusema utani huo. Staa huyo AC Milan, alisema wachezaji wa Real akiwemo Cristiano Ronaldo —wangeweza kufanya mapenzi na Fanny kama wangeweza kuingia fainali ya mabingwa wa Ulaya.

Hata hivyo baadaye alikanusha kutoa kauli hiyo. Real hawakufanikiwa baada ya kutolewa na Borussia Dortmund.

Marafiki wanasema Balo ameumia kwa kuachwa na mpenzi wake huyo lakini amejifariji kwa kununua Ferrari mpya ya paundi laki mbili.

Credits:Bongo 5
back to top