Gadner G ameamua kuvunja ukimya na kuufafanua wosia huo kupitia TBC FM wakati alipohojiwa na mtangazaji Dan Chibo katika kipindi cha The Takeover na haya ndo mazungumzo yao...
------------------------------------
Leo nilipata nafasi ya
kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki
maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema
Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno ambayo
yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi
kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile
ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu
kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu
wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya
kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience
yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha
kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi
hapa katikati ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna
mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi
kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.
Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema
ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema
ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya
uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa
kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na
matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo
dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia
kulekule ambapo yeye alipo
Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna
G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona
yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona
kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine,
ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua
kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha
akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho
anachofanya Jay Dee sasa hivi.
Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru
Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa
Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport
nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia
tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu
anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea,
ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu
wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli
kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.
Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu
ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine
unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako
mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa
ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na
kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo
hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa
kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema
ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba
wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha
kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya
mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama
wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….
Mwisho..!