Sudan Kusini imeanza kuchimba
mafuta tena na hivo kumaliza mzozo wa zaidi ya mwaka na Sudan
uliogharimu nchi zote mbili mabilioni ya dola.
Vita na tofauti nyengine bado hazikupatiwa suluhu, lakini waandishi wa habari wanasema kuanza kuchimba na kusafirisha mafuta ni ishara njema katika uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Asilimia-98 ya pato la Sudan Kusini linatokana na mafuta.