Rais mstaafu wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela, ameruhusiwa kutoka hospitali ambako akitibiwa
homa ya mapafu yaani pneumonia kwa siku kumi.
Hali ya Bwana Mandela ilishtusha mwezi Disemba mwaka jana ambapo alilazwa hospitali kwa karibu majuma matatu kwa sababu ya ugonjwa wa mapafu na kijiwe kwenye nyongo.
Rais Zuma aliwashukuru matabibu na wauguzi kwa jitihada yao ya kumuungalia Bwana Mandela kwa uzuri.