"NIMEAMUA KUMSAMEHE LULU MICHAEL....YALIYOTOKEA NAMWACHIA MUNGU"...MAMA KANUMBA
Mama
wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth
Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa upande
wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia munguAkizungumza
katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka
mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi
kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo
humkumbuka mwanaye
Alisema kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto
kwake, mume, rafiki, kaka alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na
alimfanya kuwa karibu kwake na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo
imemfanya kuwa mpweke mpaka leo