Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde
baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa
Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la
Arusha, Tanzania.Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya
maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo
katika eneo la Ngarenaro.
Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.
Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.
Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu.
Endelea kuwa nasi kwa taarifa moto moto.