Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na
wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa mahakamani baada ya kukaa
rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27,
2013.Mbele ya hakimu Joyce Msofe na mawakili Kimomogoro na
Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi
linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha
kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo
wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na
anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”
Mtuhumiwa
Lema amekana kosa hilo.Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa
mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.
Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.
Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA. kwa maandamano makubwa