Watu wanaotumia unga laini mweupe wa sembe wapo katika hatari kubwa
ya kupata ugonjwa wa kisukari, saratani na kuwa wanene kwa sababu nyuzi
nyuzi zilizopo kwenye mahindi ambazo ni muhimu kwa afya zinakuwa
zimetolewa.
Hayo yalielezwa juzi na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Basic Element Limited, Enos Andambi kinachozalisha unga wa Umoja Super Sembe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na kiwanda hicho kukabiliana na mfumo wa bei za vyakula.
Andambi alisema watumiaji wa sembe lazima watambue kwamba ubora wa sembe hautegemei ulaini na rangi kwani kutumia unga mweupe ni hatari kwa afya kwa sababu unakuwa umeondolewa virutubisho muhimu.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Alphonce Rubuye alisema katika kukabiliana na mfuko wa bei za vyakula nchini, Kiwanda cha Basic Element Limited cha jijini hapa kimenunua tani 1,500 za mahindi ambazo zitasagisha unga wa sembe utakaouzwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Rubuye alisema tafiti zilizofanywa na wataalam zinaonyesha kuwa magongwa kama kansa,vidole tumbo na matatizo ya macho katika mri mdogo yanachangiwa na matumizi ya unga usikidhi viwango vya ubora
“Kuna mazoea yaliyojengeka hasa kwa walaji wa sembe mkoa wa Dar es Salaam kupendelea zaidi sembe nyeupe sana na laini bila kuzingatia ukweli kuwa sehemu muhimu ya virutubisho inakuwa imeondolewa a kubaki bila faida kwa afya ya mlaji,”alisema Rubuye.
Alisema Watanzania lazima wabadilike kwa kuhakikisha wanatumia unga wa sembe wenye ubora ili kujenga afya zao wanapoutumia.