Marekani ndio iliyopanga hujuma za 9/11 jengo

jengo


jengo pacha ya New York yakiteketea 9/11/2001
Kamanda wa Vikosi vya Nchi Kavu vya  Jeshi la Iran amesema Marekani ndio iliyopanga hujuma za kigaidi za Septemba 11 mwaka 2001 ili kutumia matukio hayo kama kisingizio cha kulishambulia eneo tajiri la Mashariki ya Kati.

Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan amesema baada ya hujuma za Septemba 11 Marekani ilianza kuzituhumu nchi za Kiislamu kuwa zilihusika na hujuma hizo na hatimaye ikavamia kijeshi Afghanistan na kisha Iraq.
Kamanda huyo amesema Marekani ilipanga pia kuivamia kijeshi Iran lakini haikufanikiwa kutokana na sera zenye hekima za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei pamoja na umoja wa taifa la Iran.
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 11 mwaka 200, hujuma kadhaa za zilitekelezwa Marekani ambapo watu 3,000 walipoteza maisha yao.
Wataalamu kadhaa wakiwemo wahandisi mashuhuri Marekani wamesema uchunguzi wao umebainisha kuwa hujuma za Septemba 11 zilitekelezwa na serikali ya Marekani.

back to top