Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuzuia uhalifu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP.Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova.
Pikipiki 564
 zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi
.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kovaakijaribhu mkuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nch nzima mara baada ya makabidhiano anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na  kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba.
Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
back to top