SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) katika
kukabiliana na wimbi la wafanyakazi hewa imekusudia kufanya uhakiki kwa
baadhi ya taasisi zake za ulinzi ili kujua idadi kamili ya watumishi
wake.
Hali hiyo imekuja kufuatia matukio ya ubadhirifu wa fedha na kukabiliana na tatizo la kulipa mishahara kwa watumishi hewa.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri wakati akijibu swali
la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM), Jaku Hashim Ayoub aliyetaka
kujua Serikali imekabiliana vipi na tatizo la mishahara hewa kwa kikosi
cha KMKM.
Katika swali lake, Jaku alisema kwamba katika
kikosi cha KMKM Serikali inalipa watumishi hewa waliostaafu zaidi ya
Sh18 milioni kwa mwezi jambo ambalo linaipa Serikali wakati mgumu wa
kutoa mishahara isivyo stahiki.
Akijibu swali hilo Waziri Kheri alikiri kuwapo kwa ubadhirifu huo ambao umegunduliwa kutokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambapo kwa sasa
tukio hilo linafanyiwa kazi na wahusika. ”Waheshimiwa tumepokea taarifa
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu upotevu mkubwa
wa fedha za umma katika Kikosi cha KMKM ambao hulipwa wastaafu
hewa...Hatuna wasiwasi na taarifa ya mkaguzi, lakini ripoti hiyo hivi
saa inafanyiwa kazi,” alisema waziri huyo.
Alisema ni marufuku kwa watumishi wa umma kulipwa
fedha wakati wanapostaafu utumishi wa umma serikalini na kitendo hicho
ni kinyume na sheria za utumishi wa Serikali na kuwataka watu ambao
wanawatambua wenye kufanya hayo waripoti.
katika vyombo vya sheria.
katika vyombo vya sheria.
Akijibu swali la nyongeza la mwakilishi wa Jimbo
la Chake Chake (CUF), Omar Ali Shehe aliyesema kwamba zipo taarifa
katika Kikosi cha Mafunzo tatizo kama hilo lipo, Kheri alisema Serikali
itafanya ukaguzi wa taasisi zake vikiwamo vikosi maalumu vya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.