Kipimo cha CT-Scan Muhimbili chatengamaa

CT Scan


Kipimo Cha magonjwa mbalimbali ya mifumo ya fahamu pamoja na mgongo (CT- Scan) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MN) kimetengamaa baada ya kuwa kibovu kwa karibu mwaka wote wa 2012.

Hali hiyo iliusumbufu mkubwa kwa wagonjwa waliokwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kipimo hicho na kulazimika kwenda kwenye za binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha, alisema kipimo hicho kilianza kufanya kazi   Disemba 4, baada ya kufanyiwa matengenezo.
Hata hivyo, akusema gharama halisi za matengenezo wala kifaa kilichoharibika , lakini  alisema kipimo hicho kiliharibika kwa mara ya kwanza Novemba 2011 na kutengenezwa tena Julai 2012.
Alisema  pamoja na matengenezo hayo hakikudumu muda mrefu na kuharibika tena.
Eligaesha alifafanua kuwa kilichochelewesha ukarabati wa mashine hiyo ni kuwepo kwa utaratibu ambao unataka mashine tiba zinapoharibika kufanyiwa matengenezo na kampuni iliyozisambaza.
“Kwa mfano mashine hii ilinunuliwa kutoka Uholanzi, sasa lilikuwa jukumu la yule aliyeileta kuifanyia matengenezo, ndio maana ilichukua muda mrefu kidogo kutengenezwa,” alisema Eligaesha na kuwaomba liwaomba wananchi kuendelea kuwapeleka wagonjwa wao hospitalini hapo kwa kuwa mashine hiyo ni nzima na inafanya kazi.
back to top