Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepiga kalenda kesi ya uchochezi na
wizi wa mali za Sh. milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, na mwenzake, Mukadamu
Saleh.
Kesi hiyo ilihairishwa baada ya upande wa Jamhuri kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.
Hakimu Aloyce Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 17, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Oktoba 18, mwaka jana, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumani Kweka alidai kuwa washitakiwa 49 wanakabiliwa na makosa manne na Ponda anakabiliwa na makosa matano.
Makosa hayo ni kula njama kutenda kosa ,kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kuwa Oktoba 12, mwaka jana huko Chang’ombe Markasi, wasipokuwa na sababu za msingi waliingia kwa jinai kwenye kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza, kujimilikisha kiwanja hicho hali iliyosababisha uvunjifu wa amani.