
Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa Kinondoni.