Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz 'akijidai' ndani ya ukumbi wa Club Billicanas.
Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha
wasanii wanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta,
Dar, Diamond hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo
lililozua kizaazaa.Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini hakufanya hivyo.
Awali Diamond alipanda stejini mishale ya saa 8:00 akipishwa na msanii kutoka Sauz, Jigger ambaye alikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti kwa Mbongo Fleva huyo.
Wema Sepetu akihojiwa na mmoja ya watangazaji katika ukumbi wa Billicanas.
Msauz huyo alifanya shoo ya dakika 20 kisha akampisha Diamond ambaye
aliingia na Kibao cha Uswazi Take Away Remix, ambacho ndani yake
amemfagilia Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye ni hasimu wa mpenzi wake,
Wema.Baada ya kumaliza wimbo huo ndipo baadhi ya mashabiki wakasikika wakimwambia Diamond ampandishe Wema la sivyo watakinukisha.
Diamond akigonga shoo.
Ishu hiyo iliendelea hadi jamaa aliposhuka stejini hapo.Wakati Diamond akiendelea kufanya makamuzi yake hayo, Wema na Halima Kimwana wote walikuwepo ukumbini hapo na kwa bahati nzuri kama si mbaya walijikuta wote wakimshangilia Diamond, tena wakiwa VIP ya juu ambapo walikuwa wakiingia watu maalum.
Mwanahabari wetu aliwashuhudia wawili hao walipogeukiana kila mmoja alionekana kumwekea mwenzake uso wa mbuzi.
Nyomi ya kufa mtu.
Hali hiyo ilidumu hadi Diamond alipomaliza shoo yake na Wema kushuka na kumuacha Halima Kimwana.Baada ya shughuli za shoo Diamond alibaki na Halima Kimwana wakicheza disco.
Kufuatia hali hiyo kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo, kuliibuka maneno mengi kutoka kila upande kuwa shoo ya Diamond ilichafuliwa na Wema na Halima Kimwana ambaye alidaiwa alijipanga kwenda kumfanyia fujo Wema kwa kuwa yupo upande wa Penniel Mungilwa ‘Penny’.