MTITU AGOMA KUMCHEZESHA MKEWE MUVI

 
BOSI wa Kampuni ya Five Effects, William Mtitu amefunguka kuwa kamwe hatamchezesha mkewe muvi kwa madai kuwa anaogopa vishawishi vya kusalitiwa.

 
Bosi wa Kampuni ya Five Effects, William Mtitu akiwa na mkewe.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Mtitu alisema kuwa anakubali kuwa mkewe ni mrembo na anaweza kucheza filamu lakini kutokana na uzoefu wake kwenye tasnia ya filamu, anatambua vishawishi vinavyochochea michepuko ni vingi.
“Daah! Sanaa ina vishawishi sana, wapo wanaonishauri kumchezesha mke wangu lakini mimi nina uzoefu katika sanaa, siwezi kumruhusu,” alisema Mtitu ambaye ana miaka miwili ya ndoa.
back to top