Msanii wa filamu Bongo, Salma Salmin ‘Sandra’ akilia kwa huzuni baada ya kifo cha Adam Kuambiana.
KUFUATIA kifo cha msanii mkongwe wa filamu Bongo, Adam Kuambiana, msanii mwenzake, Salma Salmin ‘Sandra’ amewataka wasanii kubadili mfumo wa maisha na kumrudia Mungu.
Baadhi ya wasanii na jamaa wa karibu wa marehemu Adam Kuambiana wakiuchukua mwili.
Akizungumza na paparazi wetu katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge
jijini Dar ulipokuwa mwili wa Kuambiana kabla haujahamishiwa Muhimbili,
Sandra alisema ameumizwa sana na kifo cha msanii huyo kwani kimekuwa cha
ghafla sana hivyo ni fundisho kwao wasanii kwamba wanatakiwa kumrudia
Mungu na kuwa watu wa sala muda wote kwani kifo kipo na hakina muda
maalum.Aliongeza kuwa haifai wasanii kuwa na mabifu ya kijinga badala yake wapendane kwani hawajui kifo kitawakuta wakiwa wanafanya nini.